Kioo
Sheng' Mtaani

Zuchu ni example fiti ya wasanii wanacraft ngoma iko na mhidden message.

Si siri, kuna artists hupitisha ka-meso fulani through their work. It works across all spheres of life. Mode mwenye huenda church atafunza watoi morality, aki-use compass ya church. Rapper mlevi ata-praise pombe na madre. Mchoraji pervert atakuwa na such a message through his/her craft.

Hii ndio reason ya hii article ya leo. Nimedraw inspiration sana from two Bongo Flavor artists, Zuchu na Diamond Platnumz. Unlike many hip hop na Gengetone artists, these two hide their messages, especially if it is sexual.

The importance ni ati, hizi songs zitasikizwa na people of all ages, especially kama wanaezamake meaning out of it. Contrary to this fact ni ati, Gengetone, as much as it has all the good side ya kuget mavijanaa waks na ku-amplify movement ya kuplay Kenyan music, sometimes lyrics huwa chafu kupindukia.

With freedom of expression, msanii anafaa kuconsider song yake itasikika all over the country. Ukipita mitaani, si news kusikia mtoi wa five years akiimba phrases za “lamba lolo,” au ata “Morio kwani hupendi Vagina?”

Msanii anafaa kukaa chini na kuchora lyrics, employing stylistic devices, coz a song is poetic, and hutumia language. Ni language hufanya song inanice, as much as beats zinasaidia. Mesaage is even more important.

Before Diamond akuwe superstar mtajika, alikuwa na lyrics nzito design haina example. Dem days, his songs zilikuwa tu love language. In one of the songs, Nitarejea, anaishia safari kusaka hustle atleast mamaa na wakidi wapate kaunga. Anajua mamaa anaezakujiwa na maguyz hupitanga na mawife, ndio anamshow, “usijali ila naomba chunga sana, ogopa na marafiki,wakikulagai ata wakuambie guza mtama, waambie sidanganyiki.” In short, the hidden message ni, anam-warn against kugawa time yeye hayuko around.

The first time I heard Zuchu, morio nilibambika vibaad sana. The way io song, sukari iliandikwa, ni evidence overwhelming that alitake time kucraft lyrics zake. First of all, aliassociate lungula na sukari, kitu watu hutumia in everyday life.

Anasema “baba chanja, baba chanja,” ecidence that hii sio sukari ya kuwekwa kwa chai. It is important to note that Zuchu ametumia stylistic devices kadhaa kuongeza ladha kwa song yake, na more importantly kuongelea topic wasee wengi hushy from talking about, in contemporary Africa.

Kama kuna advice naezapiga msee out there, ni atumie izi devices kudress body ya art yake. Hizi samoo hureflect sana on who we are. Nikimada, tuchangamke kumake beautiful art. Ikibidi, tupunguze makali by hiding the messages in our craft, kama ni necessary.

By: Brian Khavalaji

Related posts