Kioo
Sheng' Mtaani

Movie Mpya ya Netflix ‘I Care a lot’ ni Lesson Biggie Kwa Raia Ku-take Care Maperoo

Kuna movie mpya in town na sijaipenda kabisa. Sijawahipenda book au movie yenye villain mbona au main character anadedi/kuuliwa.

But all in all, unaezaget lessons moja au mbili, depending na design utaview movie yenyewe.

Produced by Netflix, hii movie focus yake ni boss girl fulani msociopath vinomaa anatambulika kama Rosamund Pike(Stage name Marla Grayson). Kwa hio cinema, boss lady ni rogue lawyer na anajiita ‘legal guardian.’

Rosamund Pikes hupiga miradi na arif wake Sam Rice(Damian Young) mwenye hu-own home ya kuchunga elderly people. Hao majamaa huwa  mababi. Marla Grayson huitaji recommendation ya nurses ati hao wazee wanahitaji care. Then judge humgrant io chance ya kukuwa legal guardian. After that, huyo kikongwe atapelekwa kwa homecare ya Sam Rice. When kila kitu imesettle, Sam atapewa a piece of the pie.

Then Marla aanze kusteal assets za hao watu. Ako so extravagant. Anajilipa vinono huku the rich old people wakipewa substandard care.

Hii legal guardianship ndio main highlight ya hii movie. Iko so comedic walai. Lakini twist ya mwisho ndio imeacha viewers wengi na questions.

After kutake legal guardianship ya matha mmoja, Marla anajitia kwa noma. Mtoi wa huyo masa ni a known drug lord. The mafia comes for her. But anamshinda kwa ujanja. In a plot twist, mafia anaambiwa ni either alipe Marla ndio mamake atolewe kwa home are, or kiumane.

Wanaamua kupatner, waanzishe companies kibao, Mafia akiwa investor. Marla Grayson anakuwa star. Anapata media attention.

Then one day after show, msee anamshoot. Anadedi. Movie inadie moments later.

Lesson biggie nimelearn kutoka kwa hii movie ya Netflix ni kutake care wazazi. Hii itapunguza exploitation from rogue people. So ukiweza, fanyia mzazi kitu anakufanyia.

By: Brian Khavalaji

Related posts