Kioo
Sheng' Mtaani

Kuinvest In Yourself Ni Decision Biggy Unaezamake kama Youth

Kama unakuanga macho, lazima umesikia hii phrase ya kilami, “invest in yourself,” ama hii, “Investing in yourself is the best decision.” 

Izo sio words tu. Ziko na weight kibao. Io ndio reason imefanya tupige kambi hapa leo tuchanuane kuhusu investing in yourself.

Hii day, Wenoo tarehe 24, March 2021, niliishia Hillpark Hotel, Upperhill, kuchapa video interview fulani. Kuna mzito alikuwa on set akituchapia fitness journey yake. One important thing nilipick ni ati, wellness inadai kujituma. Inataka msee akue na descipline. Na hii yote inaboil down to kuinvest on you.

Acha nichambue hii story further.

Kuna mdem fulani ako overweight (acha nitumie hio sensitive word ju nadai kuexplain samoo fulani interesting). Huyu madam ilibidi aanze kuenda gym(hapo Hillpark) ju ni mbiggy adi kutembea ni ngori. Gym amemhelp kupunguza weight, close to 45KGS hivi in 3 months. Huyu ni mtu aliamua kuinvest kwa wellbeing yake, hapa ikiwa ni physical na mental.

Kuinvest haimean tu kuweka mullah place italeta refund. Kuinvest inamean kulearn ma ku-unlearn. Kutake risks. Kujitoa kwa comfort zone na kuexperience fullness ya life. Inamean go go out, kuchangamkia works yako na kuimprove job yako continuously.

Wiki kadhaa zimeondokea niliinterview Rina Hicks, investment banker na pia certified professional coach. Rina alinichanua on this same topic.

Alinipiga advise ati, kuinvest in yourself ukiwa myoung ni kitu imeweza sana. Alinishoo alimake mistakes horrible na kibao akiwa myoung. Akiwa campoo, alipewa pesa kibao imtake for a while then aanze kujisort. 

Rina naye ni nani? Akitumia io winch kwa food fancy na stuff kama hizi. Within no time, mamaa alikuwa hana adi dooh ya kubuy mkate pekee. Angekuwa Kenya labda angefika adi kwa mathee ashikishe chapoo mbili beans, but alikuwa majuu.

Hii story ilifanya Rina aanze kucheza na rada. Aanze kutafuta design yenye atajisave. Kumanage dooh ndio ilikuwa byproduct ya izo mistakes alimake. Today, anasaidia wasee kumake financial desicions na kumanage wealth. Rina Hicks aliinsist that ukianza kuinvest on yourself by now, miaka kumi inacome wewe utakuwa expert kwa field Yako na clients watakusaka kama vaccine ya corona.

Nikikafunga, I hope umelearn one-two. Jiinvestie ndio ureap big.

By: Brian Khavalaji

Related posts