Kioo
Sheng' Mtaani

Hustle yako itashika vinoma ukitumia hizi working tips.

Jana, Wed March 10, 2021 kulikuwa na event jamo pale Riara Uni. Io event inakuanga every once a year, kucreate awareness about clubs.

Kunakuanga na fun activities, mdemo na muziki. Pia mastudee hupata chance ya kupush hustle yao kwa kudisplay stuff wanauza au services wanaoffer.

Niliattend io event nakalearn alooot. Na purpose ya hii article leo ni kukuchanua pia ukuwe kwa limelight.

Ntatumia example ya madam fulani anaitwa Shiro. Huyu ngeus anatengeneza na kuuza lip balms. Kitu moja ilinistrike vinoma ni vile amepiga branding na vile anafanya packaging.

Branding naezasema ni vile msee anajibeba hustle yake. From the logo, to vile ana-operate, to vile social media yake inakaa. Packaging nayo ni kuwrap na kuprotect bidhaa.

Now, Shiro amejibrand vinoma. Anatumia tutubes tudogo kuweka lip balms. Then kuna kasticker hapo hivo nje ya tube. Plus a ‘thank you for doing business with us’ note, yenye pia inawork kama business card yake.

With it, mzito anaezabuy lip balm, then akidai kuipata later, anacontact Shiro kikipchoge. With this strategy, Shiro anasatisfy customers wake, plus kujimarket videadly. And the good thing is, pia wewe unaezajijenga io design.

Hustle hudai kujitolea na kusucrifice. Kuinvest kwa hustle yako itakujenga vinoma sanaa. Najua mguyz mwenye alianzisha biz place kulikuwa na compee sana Kama unajua Juju sio news kwako ati kuna PS shops kibao. Huyu mzito alikuwa analipa rent ya 7k yet dooh anapata from biz haifiki ata io 7k. But with time, bizna iliweza mbaya.

Lesson ingine noma nimelearn leo ni ati ukiwa na hustle, kuwa na business cards. Morio hii samoo inaokolea, especially ukiishia places unadai kujenga connections. Hawa majamaa unanetwork nao ukiwajenga business cards zako, ndio potential customers.

Nikifunga hii jamvi, tumecheki design kuinvest kwa biz yako inaezakukuokolea vinoma. Piga grind. Brand yourself na ustrive kusatisfy customers wako na with consistency, success itacome through.

By: Brian Khavalaji 

Related posts