Kioo
Sheng' Mtaani

Connections Utaneed 10 Years From Now Ni Squad inakusurround Sahii.

Naspent a lot of time pale LinkedIn nikisaka wasee wenye tunahsare interests. Hapo LinkedIn, hawa machampee wanaitwa connections. However utaiangalia, one way or the other, kuna time kwa life ya your s utahitaji hizi connections.

Nikigrow up nilikuwa msee msilent sana. Ilikuwa hard kumake friends. Upto the age of 18, mapero walikuwa wanatry hard sana kufigure out what kind of a kid nilkikuwa. Hii kwa ilikuwa strange. So anytime niliwashoo, “ Nimetoka kutembelea Karl.” Then mkoro aulize, “Karl ni nani.” Ile moment to nimemshoo Karl ni arif, masa alifurahi. 

Hii scenario imeniteach lesson biggy sana. That kwa life, unahitaji friends. Na si friends tu. Friends wenye wanaezacome through ile time unadai kuanzisha biz, wainvest. Friends wanaezakukutoa kwa ngori. Friends unaezapiga nao plans za kujijenga. Connections!

Hardlife Muhamba huchorea potential employees CVs na Resumes. Wacha tumchukue kama Connection. Smile Mahishi ni champee fulani alikwa anasaka works, akaenda kwa Hradlife amsaidie kujenya CV. To Smile, Hardlife ni connection. On the other hand, after Smile amejengwa wera, alisaidia arif mwingine, tumuite Mary, kuget wera. So kwa hii instance, sio tu about kukuwa kind, but kumake the right connections. Mary akitaka services za kuandimiwa CV au kucoachiwa about career now that amepata job, msee wa kwanza kuchapia ni Smile. Na because smile hayuko na expertise kwa hio field, atamrefer kwa Hardlife, mwenye hio ni profession yake.

Kama tu vile masangu alikuwa anafurahi kujua niko na beshte, kuwa na connections ni kitu ya kuleta sherehe. For the past three months, nimekuwa nikifanya documentary about period povery. As a journalist, part of the kuwork ni kusaka interview sources.Inakaa rahisi until ushike simu uanze kucall wasee. Wengine watakupromise never to show up. Others hawashiki. Emails utatuma msee! Bila the right kind of contacts, io works haingeweza.

So nilicall machampee wangu wenye najua wanapiga works arount my area of interest. From them, nikapata contacts important. Connections. From hawa wasee ilikuwa easier kuget interview sources. Na hivo ndio documentary yangu ilikuwa succesful.

Nikimada tu ni kuwachorea, 1o years from now utaneed wasee important wacome through. Utawatoa wapi kama squad yako pekee haiweziitikia io call? Jijege, ukijenga connections as ealy s sahii.

By: Brian Khavalaji

Related posts