Kioo
Sheng' Mtaani

Babysitting Imefanya Boychild Aogope Ku-marry.

Kama kuna kitu imefanya ni-rethink swala kuu la marriage, then ni babysitting. Kuna tu vitu mob zenye zinafaa kufanywa na siko  ready. Alafu si mlisema ati tunafaa ku-share roles?  I hope hii ya babysitting haiko. But anyway, that’s not important at the moment.

So hapa home raia yote imejitoa. Bro anaenda chuo. Fadhela anampeleka. The other bro ako raima na  siz pia. Mkoro  naye anaenda works. Mtaani nabaki na  Jasmine, mkidi  wa sister ya mathee. Instructions ziliachwa na Bensouda wa hii boma(mathee) ni  ati,nimake sure nimemuosha, amekula na  nichunge asipepee(Huyu mtoto husneak home anyhowly) .I thought it was easy.

I am not new to babysitting by the way. In 2017 yours truly nilipandishwa cheo, nikapewa  crown ya kukuwa acting babysitter. Those times msista wangu alikuwa a few months old. So kumlisha, kumbadilisha nguo, kumuosha, was part of my daily routine. During those days, napkins ndio zilikuwa popular, at least from where I was residing . Io  works ni calling, sio ya kila msee.

Kitu unafaa kujua ni ati, sina a close relationship na Jasmine, because home nimekuja tu for Christmas. So ilifaa nikuwe  the good guy and maybe strict kidogo. The first thing I noticed ni  ati  Jasmine hakuwa anarespond nikimuongelesha. So I thought I was harsh. Nikavaa mask  ya  upole, nione kama tutapatana. Kumbe Jasmine hakuwa anachew mandazi alipewa for brekoo. Zilikuwa zimesindiliwa kwa mdomo. How was I to deal with that?

Second thing, Jasmine hupotea tu kama  kashetani fulani. Jana, fathela alimpata some 500 m away from home. So leo  I was so alert. But even with that, sometime nikisoma Power of Shadows ya  Erin  Hunter, mtoi alijipa shughli. I looked  around mtoi alijitoa akaenda zake. Nilimpata kwa rodi, some few yards kutoka hao. Nikamshow kwa kipole, design si poa kutembea tu ovyo.

Jasmine ni mjanja. She told me ati, “nataka kuenda kucheza na Sharoo.” Nikamuuliza kwa kina Sharoo ni  wapi. Akapoint na mdomo. So nikajiambia, if toto wantii,toto getii! Nikajifanya follower wake, nikifuata steps zake ndogondogo. After like 300 yards, nikamuuliza kwa akina  Sharoo ni  wapi, Jasmine akageuka na kupoint na  mdomo. I realized nimecheswo and so we went back.

These events zilihappen before 11 AM. I wasn’t prepared for it. But I gained something. For example, kuenda kwa  akina  Sharoo,who was kinda fictional, ilikuwa tizi  for me. I rarely do that. I also learned, mimi na  Jasmine hatupatani. However, I could read her facial expressions and know when she was mad. That way, nilikuwa nacheza kama mimi, even though nilikuwa naboeka. Finally, I understood why mkoro alikuwa anatunyorosha viboko tukiwa watoi; Ni hizi tabia tu.

So, 2021 imeanza fiti. But utu tu-small challenges twa babysitting tumenifanya ni-rethink when I should get married, which was set to be on… (Scratch here). Otherwise, I welcome tips za babysitting, hivi karibuni naezakuwa fathela.

By: Brian Khavalaji

Related posts